Skip to main content

Mashirika ya WFP/WHO yahudumia kihali raia waathirika wa mapigano Sri Lanka

Mashirika ya WFP/WHO yahudumia kihali raia waathirika wa mapigano Sri Lanka

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa ilani inayohadharisha kwamba pindi halitafadhiliwa msaada wa dharura wa dola milioni 40, kuhudumia chakula umma ulioathirika na mapigano katika Sri Lanka, litashindwa kununua chakula, kuanzia mwisho wa Julai ili kunusuru maisha ya wahamiaji.

 Hivi sasa WFP imeweza kupeleka misafara mitano ya tani 150 za chakula, shehena ambayo inabashiriwa itamalizika katika siku tano zijazo. Kadhalika, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa limenyimwa uwezo na fursa ya kuyafikia yale maeneo ya mapigano, na kufanya ukaguzi wa afya ya raia walionaswa kwenye mazingira hayo. Wakati huo huo WHO imeleza hospitali ya muda, inayosimamiwana UM, iliopo karibu na eneo la mapigano inatoa huduma za afya zisioridhisha, kwa raia muhitaji, kwa sababu ya upungufu wa vifaa na madawa.