Makundi yanayopigana Sri Lanka yatakiwa kuhishimu usalama wa raia

12 Mei 2009

Verinoque Taveau, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) aliwaambia waandishi habari Geneva kwamba makundi yanayopambana katika Sri Lanka, yaani vikosi vya Serikali na waasi wa kundi la LTTE [Tamil Tiger], yamenasihiwa na UNICEF kufanya kila wawezalo kuwahakikishia raia ushoroba wa kupita, bila ya kushambuliwa kwenye mazingira ya uhasama.

 UNICEF pia imeeleza kuongeza misaada ya kihali, ikijumlisha maji safi ya kunywa, kwenye zile kambi za wahamiaji wa ndani na inajitahidi vile vile kuwapatia lishe bora waathirika watoto wanaosumbuliwa na tatizo hatari la utapiamlo katika eneo la mapigano.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter