Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanakijiji wa Kenya wadhaminiwa mradi wa kudhibiti kaboni kwa natija za mazingira

Wanakijiji wa Kenya wadhaminiwa mradi wa kudhibiti kaboni kwa natija za mazingira

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limeripoti kuanzishwa mradi wa maendeleo wa kuwashirikisha wanavijiji kutoka Kenya magharibi ili kutunza vyema mazingira yao.

 Mradi huu unadhaminiwa na UNEP pamoja na wadau wengine wa kimataifa, na utatumiwa kutathminia kiwango cha kaboni inayokusanywa kwenye miti na udongo na namna kadhia hii itakavyosaidia kudhibitiwa kwa taratibu za kusarifika, zitakazotumiwa kuimarisha zaidi hifadhi ya mazingira. Mpango huu, utaojulikana kama Mradi wa Faida ya Kaboni (Carbon Benfits Project) ulianzishwa rasmi siku ya leo na UNEP, ikishirikiana na Taasisi ya Kilimo cha Misitu Duniani pamoja na ile taasisi inayojilikana kwa ufupi, Taasisi ya GEF. Taassi ya GEF ndio iliofadhilia fedha za mradi. Jamii nyengine zinazotekeleza mradi kama huu hukutikana katika mataifa ya Niger, Nigeria na Uchina, ambapo wanasayansi huko wanabuni mfumo wa kisasa utakaotumiwa kupima, kufuatilia na kusimamia kaboni na taathira zake kwenye mazingira, kwa kulingana na Mkataba wa UM juu ya Udhibiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Mkataba wa Kyoto. Mikataba hii ilipendekeza kwa mataifa yenye maendeleo ya viwandani, kufidia uharibifu wa mazingira duniani unaochochewa na umwagaji wao wa hewa chafu angani, kwa kufadhilia nchi zinazoendelea fedha za kuimarisha miradi ya kutumia nishati safi, na ya kutumiwa mara kwa mara, ili zidhibiti vyema kaboni kwenye mazingira yao anuwai.