Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki ya kupata chakula ni haki msingi ya kiutu, asisitiza De Schutter

Haki ya kupata chakula ni haki msingi ya kiutu, asisitiza De Schutter

Olivier De Schutter, Mkariri Maalumu juu ya haki ya chakula ameiambia Kamisheni ya UM juu ya Maendeleo Yanayosarifika kwamba umma wa kimataifa unalazimika kuandaa, kidharura miradi madhubuti itakayoimarisha na kudumisha mifumo ya kuzalisha chakula kwa wingi, kwenye mazingira ya ulimwengu wa sasa, mazingira yaliokabiliwa na madhara kadha wa kadha yanayochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa na kupungua kwa maliasili duniani.

Alihadharisha ya kuwa bila ya mataifa kutambua ule ukweli uliothibitishwa kimataifa, kwamba mtu kupata chakula ni moja ya kanuni ya msingi ya haki za binadamu, hatutoendelea kufanikiwa kulikomesha tatizo la chakula ulimwenguni. Alisisitiza bayana hii ni lazima kujumlishwa kihakika kwenye sera zote za maendeleo ya kilimo.