Skip to main content

UNHCR kutoridhika na kurejeshwa Libya wahamiaji kufuatia mabishano kati Malta na Utaliana

UNHCR kutoridhika na kurejeshwa Libya wahamiaji kufuatia mabishano kati Malta na Utaliana

Imeripotiwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kuna wasiwasi mkubwa miongoni mwa jumuiya ya kimataifa kuhusu usalama wa watu 230, waliookolewa Ijumatano na motoboti za doria za Serikali ya Utaliana, kwenye Eneo la Ukaguzi na Uokoaji la Malta, ambalo hujulikana kama eneo la SAR.

Wahamiaji hawa 230 walirejshwa Libya Ijumatano bila ya idhini yao, na bila ya kutathminiwa au kufanyiwa makadirio ya hali halisi wanaokabiliwa nayo, na kama wanahitaji hifadhi ya kisiasa. Wahamiaji waliokolewa kwenye eneo la maili 35 za kibaharia, kusini-mashariki ya kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa, eneo ambalo lipo, kisheria, chini ya mamlaka ya Malta. Uamuzi wa kuwarudisha wahamiaji Libya ulifanyika baada ya kuzuka mabishano makali baina ya wawakilishi wa serikali za Malta na Utaliana, kuhusu nani mwenye dhamana ya kuwaokoa wahamaiji waliobanana kwenye mashua tatu, zilizokabiliwa na hatari ya kuzama. Asili za wahamiaji hawa, wakati tulipoelekea studio, zilikuwa bado hazijatambuliwa.