Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya FAO/WHO/OIE yakana virusi vya H1N1 huambukiza watu wanaokula nguruwe

Mashirika ya FAO/WHO/OIE yakana virusi vya H1N1 huambukiza watu wanaokula nguruwe

Mashirika matatu muhimu ya kimataifa yanayoshughulikia afya na chakula, yaani Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) yametangaza taarifa ya pamoja yenye kuthibitisha kwamba vimelea vya homa ya mafua, kikawaida, haviambukizi wanadamu kwa kula nyama ya nguruwe au vitu vinavyotokana na nguruwe.

 Ilani ya mashirika ilisisitiza nyama ya nguruwe inayopikwa kwa kipimo cha digrii za sentigredi 70 au nyuzijoto 160 za Farenhaiti, na ziada, huangamiza uwezo wa virusi vya maradhi kudhuru wanadamu. Lakini taarifa ya mashirika haya matatu ya kimataifa vile vile imehadharisha kwamba wanaohudumia biashara ya nyama ya nguruwe yanalazimika na kuwajibika kuhakikisha wanatumia utaratibu mzuri wa usafi ulioshauriwa na Shirika la WHO.