Skip to main content

Mapigano Sudan kusini yazusha wasiwasi juu ya usalama wawatoto:UNICEF

Mapigano Sudan kusini yazusha wasiwasi juu ya usalama wawatoto:UNICEF

Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa na wasiwasi kuhusu madhara, yakiakili na mwili, wanayopata watoto wadogo kutokana na mapigano yalioselelea kwenye majimbo kadha ya Sudan Kusini.

UNICEF ilitoa mwito maalumu kwa makundi yote yanayopigana, kujizuia na vitendo kama hivi, na kuhakikisha watoto wote huwa wanapatiwa ulinzi bora, na pia kuruhusu mashirika yanayohudumia kihali watoto kuendeleza kazi zao bila ya vizingiti, ili kunusuru maisha ya fungu hili muhimu la raia.  Mwito huu, kwa mujibu wa UNICEF, unalingana na Mkataba wa UM juu ya Haki ya Mtoto.