Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa tahadhari ya mapema maafa unafanyiwa mapitio na wataalamu wa WMO

Mfumo wa tahadhari ya mapema maafa unafanyiwa mapitio na wataalamu wa WMO

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeripoti wataalamu 90 kutoka nchi wanachama walikutana kwenye Makao Makuu ya Geneva, kutathminia ubora wa hewa na mabadiliko ya hali ya hewa yaluiojiri ulimwenguni pamoja na athari zake.

Kadhalika kwenye mkutano kulizingatiwa mfumo hakika wa mazingira ulivyo kwa sasa katika dunia. Taarifa ya WMO kuhusu mkutano ilikumbusha tena umuhimu wa kuwepo miradi ya kimataifa inayotumiwa kutahadharisha mapema matukio ya ajali za kimaumbile.  Takwimu za WMO zinaonyesha mnamo kipindi cha nusu karne iliopita, idadi ya maafa na hasara za kiuchumi ulimwenguni ziliongezeka kwa kiwango kikubwa, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya vina vya maji duniani. Lakini kwa wakati huo huo, ilitiliamkazo ripoti ya WMO, viwango vya upotezaji wa maisha viliteremka mara 10 ulimwenguni, kwa sababu ya kutumika kwa miradi ya kutabiri mapema maafa, iliohadharisha na kuokoa asilimia kubwa ya maisha umma.