Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya Utafiti wa Sayansi yakutana Geneva kuzingatia chanjo kinga dhidi ya virusi vya H1N1

Kamati ya Utafiti wa Sayansi yakutana Geneva kuzingatia chanjo kinga dhidi ya virusi vya H1N1

Kikao cha pili cha Kamati ya Utafiti wa Kisayansi, kilichoongozwa kimataifa kutokea ofisi za UM za Geneva, leo jioni, kilikusanyisha wanasayansi na matabibu 150, kutoka sehemu mbalimbali za dunia, ambao walishauriana, kwa kutumia njia ya vidio, masuala kadha wa kadha kuhusu utaratibu unaofaa kuchukuliwa kidharura kutengeneza chanjo ya kudhibiti vimelea vya homa ya mafua ya A(H1N1), na kuzingatia kiwango halisi cha maambukizi ya maradhi duniani kwa sasa.

Vile vile kikao kilitathminia mfumo wa virusi ulivyo, kipindi cha vijidudu kupevuka, na kujaribu kupima makali ya maambukizi na pia kusailia kundi lipi la wanadamu huathirika zaidi na virusi vtya H1N1 na kwa nini. Matokeo ya uchunguzi wa majadiliano ya wataalamu wa Kamati ya Kisayansi yanatarajiwa kutangazwa rasmikatika siku za karibuni.