Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ahimiza ushikamano wa kimataifa kupambana na homa ya H1N1

KM ahimiza ushikamano wa kimataifa kupambana na homa ya H1N1

Kwenye mahojiano ya kila mwezi na waandishi habari wa kimataifa, yanayofanyika Makao Makuu ya UM, KM Ban Ki-Moon aliwakumbusha tena walimwengu juu ya fungamano hakika zilizidhihiri miongoni mwa mataifa katika nyakati za sasa. Kwa hivyo, alisihi Mataifa Wanachama kujitahidi kushirikiana kipamoja kudhibiti vyema mripuko wa virusi vya homa ya mafua ya H1N1, hali itakayoleta nantija kwa wote pote duniani.

 Alisisitiza kwamba "tishio lolote la afya linalotochochewa na miripuko ya maradhi kwenye taifa moja huathiri pia afya ya kila taifa duniani, hali ambayo haitofanikiwa kudhibitiwa kikamilifu, kama inavyostahiki, bila ya mchango wa jamii yote ya kimataifa."