Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa rasmi ya rakamu 15 juu ya homa ya H1N1

Taarifa rasmi ya rakamu 15 juu ya homa ya H1N1

Takwimu mpya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu hali halisi ya maambukizi ya homa ya mafua ya H1N1 ulimwenguni zimeonyesha ongezeko la wagonjwa 39 walioambukizwa na homa ya mafua ya A/H1N1.

Fadela Chaib, msemaji wa WHO, aliarifu asubuhi mjini Geneva,  mbele ya wanahabari wa kimataifa, kwamba kuanzia saa 06:00 za majira ya GMT, nchi 21 ziliripoti rasmi kwa UM kuwa zilisajili wagonjwa walioambukizwa na homa ya mafua ya H1N1 kwenye maeneo yao. Jumla ya wagonjwa waliosajiliwa kupatwa na homa hiyo imeongezeka kwa wagonjwa 39, na takwimu mpya inajumlisha wagonjwa 1,124 wa homa ya H1N1 kimataifa. WHO ilisema ongezeko hili la wagonjwa waliopatwa na homa lilitukia katika Kanada.