Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BK lakutana kusikiliza ripoti ya maendeleo ya KM kwenye udhibiti wa homa ya A(H1N1)

BK lakutana kusikiliza ripoti ya maendeleo ya KM kwenye udhibiti wa homa ya A(H1N1)

Leo asubuhi, kwenye Ukumbi wa Mikutano, wa rakamu ya tatu, kulisanyika wajumbe wa kimataifa kwenye kikao maalumu cha wawakilishi wote, kusikiliza fafanuzi za KM Ban Ki-moon, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dktr Margaret Chan juu ya maandalizi ya kimataifa ya kudhibiti bora mripuko wa virusi vya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1).