Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kuadhimishwa na UM Ijumapili - 03 Mei 2009

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kuadhimishwa na UM Ijumapili - 03 Mei 2009

Tarehe 03 Mei huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni Sikukuu ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Kwenye risala iliowakilishwa na KM Ban Ki-moon kuihisihimu siku hii aiwapongeza wanahabari wote wa kimataifa, wenye kuendeleza shughuli zao kwenye mazingira magumu kabisa, kwa lengo la kuhakikisha walimwengu huwa wanapatiwa taarifa za habari zilizo huru, za haki na zisiopendelea. Risala ya KM iliyahimiza Mataifa Wanachama kuhakikisha wanahabari huwa wanapata hifadhi na usalama unaostahiki kutekeleza majukumu yao. Alisisitiza kwamba vyombo vya mawasiliano ya habari, vilivyo huru, ndio vifaa vinavyohitajika kuwepo kimataifa, kwa mintarafu ya kuimarisha haki za binadamu, kukuza maendeleo yenye natija kwa umma wa kimataifa na kudumisha amani ya dunia.