Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM inaitaka Israel ikomeshe kubomoa nyumba za Wafalastina Jerusalem mashariki

UM inaitaka Israel ikomeshe kubomoa nyumba za Wafalastina Jerusalem mashariki

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imewakilisha ripoti maalumu ya kurasa 21 kuhusu hali ya raia wa KiFalastina, waliong’olewa makazi na wenye mamlaka wa Israel, kwenye eneo la Jerusalem mashariki.

UM imependekeza kwa Israel kuwacha kubomoa zile nyumba za WaFalastina wanaoishi kwenye mji wa Jerusalem mashariki, na paop hapo pia kuwataka wenye mamlaka kushughulikia kidhati mzozo wa ukosefu wa nyumba unaoendelea kuongezeka kila kukicha, na kusumbua wakazi WaFalastina wa Jerusalem. Kwa mujibu wa ripoti ya OCHA darzeni za nyumba za WaFalastina huwa zinabomolewa, na kuvunjwa, kila mwaka na wenye mamlaka, kwa kisingizio nyumba hizi zimekosa vibali vya manispaa juu ya upangaji wa miji.  Wapinzani wa vitendo hivi wanasisitiza kwamba hatua za kubomowa nyumba za WaFalastina, zinazochukuliwa na Israel, ni miongoni mwa mizungu ya wenye madaraka kutaka kueneza na kupanua zaidi udhibiti wa maeneo hayo, na baadaye kuwaweka huko wale walowezi wa Kiyahudi.