Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makampuni ya madawa yanahimizwa na IAEA kuunda chombo rahisi kudhibiti saratani

Makampuni ya madawa yanahimizwa na IAEA kuunda chombo rahisi kudhibiti saratani

Shirka la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeyahamasisha makampuni yanayotengeneza vifaa na zana za matibabu kuunda chombo kipya cha tiba ya saratani kkitakachokuwa na nguvu, chepesi, kinachobebeka, rahisi kutumia na ambacho watu wa kawaida watamudu kukinunua.

Werner Burkart, Naibu Mkurugenzi wa IAEA anayehusika na Idara ya Matumizi ya Nishati ya Nyuklia alionya kwamba maradhi ya saratani hayatofanikiwa kudhibitiwa wagonjwa ikiwa miradi ya jumla ya kudhibiti maradhi haya haiwafikii umma masikini. Kwa hivyo, alipendekeza kwa makampuni ya kimataifa kutumia umahiri walionao kutengeneza vifaa rahisi na madhubuti vya tiba ya afya, vitakavyotumika sio katika vituo vya mahospitali ya katika miji pekee bali pia vitatuhudumiwa ule umma masikini wa vijijini na kwenye mazingira kamahayo. Mwito huu ulitolewa kwenye Mkutano wa Kimataifa juu ya Maendeleo ya Tiba ya Mionzi dhidi ya Saratani ulioanza mijadala yake Ijumane ya leo mjini Vienna, chini ya usimamizi wa IAEA.