Skip to main content

Baraza la usalama linasailia hali katika Cote D'ivoire

Baraza la usalama linasailia hali katika Cote D'ivoire

Baraza la Usalama leo limekutana asubuhi kusailia hali katika Cote d\'Ivoire.

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Cote d'Ivoire, Choi Young-jin, aliwaambia wajumbe wa Baraza kwamba kasi ilioshuhudiwa siku za nyuma, kwenye matayarisho ya uchaguzi mkuu nchini, sasa hivi imepwelewa sana, na matarajio yote ya kufanyisha uchaguzi huo hutegemea namna mradi wa muungano wa taifa unavyotekelezwa.  Shirika la Ulinzi Amani katika Cote d'Ivoire (UNOCI) limeeleza kuwa linajitahidi kuchangisha kwa kila njia huduma zao ili kusaidia mpango wa kuunganisha taifa unatekelezwa haraka.