Wakulima Afrika magharibi wanakabiliwa na athari haribifu za hali ya hewa, kuonya WMO
Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeripoti wakulima wa Afrika Magharibi wanatishiwa na hatari ya kukabwa kimaendeleo kwa sababu ya athari haribifu zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye ukanda wao.
Marudio ya mara kwa mara ya ukame kwenye eneo, ikichanganyika na mawimbi ya joto kali, mafuriko, dhoruba na baridi inayosababisha utando wa barafu pamoja na uvamizi wa nzige ni matukio ambayo yenye kuishinikiza sekta ya kilimo Afrika Magharibi kufanya marekibisho ya dharura ili kumudu vyema athari zinazochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa. Shirika la WMO, likijumuika na Shirka la Chakula na Kilimo (FAO), Idara ya Taifa juu ya Hali ya Hewa katika Uspeni (AEMET) na wadau wengine yameamua wiki hii kuwakusanyisha wataalamu 70 kwenye mji wa Ougadougou, Burkina Faso kuzingatia sera za marekibisho, pamoja na maamuzi ya pamoja yanayotakikana kusaidia udhibiti bora wa kilimo pamoja na ufugaji wa wanyama, utunzaji wa misitu na katika sekta ya uvuvi katika Afrika Magharibi.