Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaumu misaada ya ilimu ya msingi iliteremka 2007 katika nchi masikini

UNESCO yalaumu misaada ya ilimu ya msingi iliteremka 2007 katika nchi masikini

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeripoti mproromoko mkubwa wa misaada ya kuhudumia ilimu ya msingi katika nchi zinazoendelea.

Hali hii inatabiriwa itarudisha nyuma zile juhudi za kutekeleza Malengo ya Milenia yaliokusudiwa kupunguza kutojua kusoma na kuandika, kwa kuhakikisha watoto wote, wa kiume na kike, hupatiwa ilimu ya msingi. Kwa mujibu wa takwimu zilizonakiliwa na UNESCO, kutoka matokeo ya utafiti wa Kamati ya Misaada ya Maendeleo ya Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), imethibitishwa kwamba jumla ya misaada ilioahidiwa kuimarisha ilimu ya msingi katika nchi masikini katika 2006 ilikuwa sawa na dola bilioni 5.5, na katika 2007 jumla hiyo iliteremka kwa asilimia 22, na kufikia dola bilioni 4.3.