Skip to main content

ILO yaadhimisha miaka 90

ILO yaadhimisha miaka 90

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) linajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya kutimia miaka 90 tangu kubuniwa katika kipindi ambacho walimwengu hukabiliwa na mzozo mkuu wa fedha, ukichanganyika na ukosefu wa ajira.

 Taadhima hizi zitafanyika mnamo wiki ya tarehe 21 mpaka 28 Aprili (2009), katika nchi wanachama 100 ziada, ambapo umma wa kimataifa utashiriki kwenye mijadala ya kijamii mbalimbali, na kuzingatia namna ya kuzalisha ajira yenye hishima kwa wafanyakazi muhjitaji, katika mazingira ya soko la kimataifa linalotekeleza haki kwa wote. Kadhalika, taadhima hizi za Miaka 90 ya ILO zitajumlisha matangazo kadha wa kadha ya vipindi vya redio na televisheni kwa madhumuni ya kuamsha hisia za walimwengu juu ya haki za wafanyakazi. Vile vile kutafanyika warsha na maonyesho mengineyo yanayohusu ajira na vigezo vya kutumiwa kutekeleza haki za wafanyakazi kimataifa.