Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP inatayarisha mkutano wa kuzingatia upigaji marufuku madawa 12 ya kuuwa wadudu waharibifu

UNEP inatayarisha mkutano wa kuzingatia upigaji marufuku madawa 12 ya kuuwa wadudu waharibifu

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) linatazamiwa kuandaa mkutano maalumu Geneva kusailia tatizo la afya, linalosababishwa na aina 12 za madawa yanayotumiwa kuuwa wadudu waharibifu wa mazo, madawa ya kemikali ambazo husemekana zinahatarisha afya ya wanadamu na kusababisha maradhi thakili ya saratani.

 Lengo hasa la mkutano litakuwa ni kutafuta njia za kusitisha kabisa utengenezaji, na pia matumizi, ya kemikali hizi. Miongoni mwa madawa ya kuulia wadudu yatakayozingatiwa ni pamoja na ile dawa ya DDT, ambayo ilitumiwa sana siku za nyuma na wanadamu. Lakini licha ya kuwa DDT ilifanikiwa katika kudhibiti malaria, kimataifa, athari zake kiafya ni mbaya sana na ni hatari kwa wanadamu.