Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya raia waliongolewa makazi na mashambulio ya waasi wa FDLR yakithiri JKK kuhudharisha UNHCR

Idadi ya raia waliongolewa makazi na mashambulio ya waasi wa FDLR yakithiri JKK kuhudharisha UNHCR

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumanne asubuhi aliwaeleza waandishi habari mjini Geneva kwamba mnamo wiki saba zilizopita idadi ya raia waliong\'olewa makazi ilikithiri pomoni, kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya waasi wa kundi la FDLR, kwenye eneo la Lubero, Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

 Idadi hii inasemekana sasa imekiuka wahamiaji raia 100,000. Alisema mfuatano wa mashambulio ya pamoja ya waasi dhidi ya raia katika vijiji vya Luofu, Kirumba, Kanyabonga na Kayna karibu na Lubero, kilomita 170 kaskazini ya Goma, yamewacha mabaki ya msururu wa vifo na uharibifu uliokiuka mipaka, hali iliowalazimisha wanavijiji kuhama, kidharura, makazi yao . Kwa mujibu wa taarifa ya wenye madaraka ya serikali za vijijini, katika  Ijumaa iliopita waasi wa FDLR walivamia kijiji cha Luofu na kuua watu saba, ikijumlisha watoto wadogo watano. Vile vile waasi hawa imeripotiwa waliunguza moto nyumba za mashambani 255, na kuwalazimisha wakazi wa eneo hilo kukimbilia vichakani kunusuru maisha yao, wakati wenziwao wengine walikimbilia mji wa karibu wa Kirumba. UNHCR imeripoti kwamba tangu Ijumapili waasi wa FDLR wanaripotiwa kuuzunguka mji wa Kirumba, na kutishia kuuvamia na kueneza wapiganaji wao kwenye eneo.