Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon na Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu wameripotiwa kuchukuziwa na hotuba ya Raisi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mahmoud Ahmadinejad aliowasilisha Ijumatatu kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mapitio ya Mwito wa Durban na Mpango wa Utendaji wa Kupiga Vita Ubaguzi wa Rangi Duniani uliofanyika Geneva, Uswiss.

 KM alisisitiza hotuba ya Raisi wa Iran ilikuwa ni ya "kushtumu, kutenganisha na ya uchochezi" kwa umma wa kimataifa. Kwa upande wake Kamishna Pillay alidai hotuba ya Raisi Ahmadinejad "ilivuka upeo wa dhamira hasa" ya Mkutano.

Moto uliripotiwa kupamba Ijumapili kwenye makao makuu ya Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) katika mji wa El Fasher mnamo saa nne za usiku. Moto huo ulifanikiwa kudhibitiwa na Vikosi vya Wazima Moto vya UNAMID, vikisaidiwa na wanajeshi wa Rwanda na Misri pamoja na Idara ya Zimamoto ya Jimbo. Hakuna mtu aliyeripotiwa kujeruhiwa na tukio hilo. Makadirio ya awali ya athari za ajali ya moto zinaonyesha vifaa vya mawasiliano, vinavyogharamiwa dola milioni 4 viliharibiwa pamoja na pia vifaa vyengine vya ofisi, kama fanicha na maabara ya utafiti wa maji, ambavyo uharibifu wao unagharammiwa dola milioni moja. Juu ya hayo, ofisi 11 zilizotengenezewa makontena pamoja na ghala mbili za Rubb Hall nazo pia zilizharibiwa kwa ukamilifu.

Tume ya majaji watano wa Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishaji imeanza kusikiliza upya mashitaka juu ya mzozo wa uwekaji mipaka kwenye Eneo la Abyei, mgogoro unaohusu Serikali ya Sudan na jeshi la mgambo la kundi la SPLM. Hatua hii imechukuliwa kufuatilia ombi liliotumwa Kortini mwezi Julai 2008.

Shirika la UM Linalohusika na Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limeeleza kufanikiwa kuyakamilisha majukumu ya operesheni za pamoja na Vikosi vya Taifa vya Kongo dhidi ya majeshi ya mgambo yanayoranda kwenye eneo la kaskazini-mashariki. Operesheni zilizoanzishwa mwezi Januari zilikusudiwa hasa kudhibiti mabaki ya waasi wa kundi la FPRI na makundi mengine haramu yaliopo Jimbo la Kivu Kaskazini. MONUC imeripoti karibuni iliopoa maiti 11 ya wapiganaji waasi pamoja na kupokonya vifaa kutoka ghala ndogo ya silaha. Kadhalika MONUC imeeleza kuwa itaendelea kuwapatia Jeshi la Kongo huduma za lojistiki, ikijumlisha upelelezi wa anga pamoja na shughuli za kuhamisha majeruhi wanaohutajia matibabu ya dharura.

Naibu KM wa UM Asha-Rose Migiro amehadharisha kwenye hotuba, aliotoa mbele ya wajumbe waliohudhuria Mkutano juu ya Uimarishaji wa Sheria, kwamba kuna ukosefu wa mwambatano wa sera zinazohusu taratibu za kuhishimu sheria, miradi ambayo alisema hubuniwa na mashirika kadhaa yasio ya kiserikali "yaliosongomana" kikazi. Alisema mara kwa mara hukutikana uharibifu na matatizo ya kurudufu huduma za kazi. Kwa ziada, NKM aliongeza kusema, miradi inayobuniwa kusaidia kuendeleza sheria mara nyingi huwa ya "kidogo kidogo na hukidhi zaidi mahitaji ya wahisani wa kimataifa" badala ya mahitaji ya wahusika halisi wa kadhia hizo.

Jumuiya ya Mashirika ya UM Dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) imetangaza taarifa iliokaribisha kuachiwa huru wanaume tisa waliowekwa kizuizini na wenye madaraka Senegal kutokana na vitendo vya usenge/ukhanithi. Watu hawa walikuwa wanachama wa shirika la kufunza raia wa Senegal namna ya kujikinga na maambukizo ya virusi vya UKIMWI. Walihukumiwa kushiriki kwenye "vitendo vinavyokwenda kinyume na maumbile" kwa kuanzisha kile kilichotafsiriwa kama "jumuiya ya wahalifu." Kwa mujibu wa Michel Sidibé, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya UNAIDS, woga na khofu dhidi ya misenge na mabasha, pamoja na sheria ya kufanya uhalifu vitendo vya wasenge kuigiza jinsiya tofauti ni hatua zenye kuapalilia zaidi janga la UKIMWI. Kwa kulingana na sababu hizi, ndio Sidibé alilazimika kutoa nasaha inayoitaka Serikali ya Senegal kuchukua hatua za mapema, ili kufuta sheria hizo kitaifa na kupambana vizuri zaidi na janga la UKIMWI nchini.