Mkutano Dhidi ya Ubaguzi waanza rasmi Geneva

20 Aprili 2009

Mkutano wa UM juu ya Mapitio ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi wa Rangi Duniani umeanza rasmi hii leo mjini Geneva. Kwenye risala ya ufunguzi, KM Ban Ki-moon alieleza masikitiko juu ya uamuzi wa baadhi ya nchi wanachama, wa kutohudhuria kikao hiki, licha ya kuwa ushahidi uliopo umethibitisha dhahiri kwamba ubaguzi wa rangi ni tatizo ambalo linaendelea kuselelea, na kujizatiti katika maeneo kadha wa kadha ya ulimwengu.

"Tunawaza taratibu za kusonga mbele, zenye mwelekeo mpya,

Geneva kukabiliana na janga la ubaguzi wa rangi, na wakati huo huo

20/04/09 tunaendelea kushikilia yaliopita. Tunazungumzia umuhimu wa kuwa na umoja mpya, unaolingana na wakati, dhidi ya janga hili. Huku tunaendelea kugawanyika na udhaifu wa taratibu zinazobainisha ukakamavu wa tabia za kikale. Huzungumzia uvumilivu na kuhishimiana kibinadamu, na wakati huo huo tunaendelea kuonyeshana vidole na kulaumiana kwa kauli zile zile zinazowakilisha maadili ya miaka na miongo iliopita, maadili yaliopitwa na wakati. Inasikitisha na kuhuzunisha kuona baadhi ya mataifa, yenye uwezo wa kujumuisha mchango wao, kusaidia kusukuma mbele juhudi zitakazoleta natija zenye manufaa kwa wote dhidi ya ubaguzi, kwa wakati ujao, mataifa hayo yameamua kutohudhuria mkutano."

Msimamo wa KM vile vile uliungwa mkono na Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, ambaye alidhihirishwa "kushtushwa na kuvunjika moyo kabisa na uamuzi wa Marekani kutohudhuria Mkutano wa Mapitio ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi wa Rangi Duniani". Alilaumu ya kuwa kuna mataifa machache yalioamua kukabiliana na suala zima la ubaguzi wa rangi na utovu wa kuvumiliana kitamaduni, kwa kulenga lawama zao kwenye suala moja, au masuala mawili pekee, yanayoambatana na masilahi yao ya kizalendo tu!

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter