Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakaguzi wa IAEA wapigwa marufuku Korea Kaskazini

Wakaguzi wa IAEA wapigwa marufuku Korea Kaskazini

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeripoti kupokea risala rasmi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini/DPRK) inayosema kwamba kuanzia Ijumanne ya tarehe 14 Aprili, inasitisha uhusiano na ushirikiano wote na wakaguzi wa IAEA waliopo kwenye viwanda vya nishati vya kinyuklia katika mji wa Yongbyon.