Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa Haki za Binadamu kuihimiza jumuiya ya kimataifa kushirikiana kukomesha uovu wa ubaguzi wa rangi

Kamishna wa Haki za Binadamu kuihimiza jumuiya ya kimataifa kushirikiana kukomesha uovu wa ubaguzi wa rangi

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ameyasihi Mataifa Wanachama kujiepusha na alioitafsiri kuwa ni tabia karaha inayowakilisha "mawazo finyu ya kisiasa" na "ung\'anga\'niaji wa uzalendo", na badala yake kuyataka mataifa yakamilishe maafikiano yanayokabiliwa na wote, ili kuendeleza mbele juhudi za pamoja za kupiga vita utovu wa ustahamilivu wa kitamaduni na uovu wa ubaguzi wa rangi duniani.

Pillay aliitoa nasaha hii wiki hii wakati Mtaifa Wanachama katika  UM yanajiandaa kukutanika Geneva, kuanzia 20-24 Aprili, kuhudhuria Mkutano wa Mapitio ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi wa Rangi, Ukabila na Chuki ya Wageni.