Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU inashukuriwa na WFP kwa ulinzi wa misaada ya chakula kwa Usomali

EU inashukuriwa na WFP kwa ulinzi wa misaada ya chakula kwa Usomali

Ramiro Lopes da Silva, Naibu Mkuu wa Operesheni za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) ametoa taarifa maalumu, kutokea Makao Makuu ya ofisi zao yaliopo Roma, Utaliana iliyozishukuru nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa kufadhilia manowari kadhaa zinazotumiwa kuongoza meli zilizobeba msaada wa chakula wa WFP, na kuzikinga meli hizo na mashambulio ya maharamia, kitendo ambacho alisema ndicho chenye uwezo wa suluhu ya muda mrefu, itakayosaidia kunusuru umma wa Usomali na hatari ya njaa.