Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imeripoti hali ya usalama Darfur ni shwari

UNAMID imeripoti hali ya usalama Darfur ni shwari

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limeripoti ya kuwa hali ya usalama kieneo, kwa hivi sasa, ni shwari licha ya kuwepo vitendo vya uharamia na wizi wa magari katika baadhi ya sehemu za Darfur Kaskazini na Magharibi.

Kwa mujibu wa ripoti za UNAMID, katika mwezi uliopita operesheni za vikosi vya mchanganyiko vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, A  vilivyodhaminiwa  majukumu ya kukomesha fujo na vurugu, na pia kuhifadhi wa Darfur, vilikabiliwa na matatizo kadha wa kadha yalioambatana na hali ya wasiwasi kwa sababu ya mifumko ya mashambulio dhidi ya walinzi amani wa kimataifa, pamoja na uharamia ulioendelezwa na makundi yenye kuchukua silaha, ikichanganyika pia na wizi wa magari na kuchoma moto kambi za wahamaji wa ndani ya nchi (IDPs) na vile vile unyanyasaji wa kihorera wa raia. Vile vile katika kipindi hicho, iliripotiwa kuwepo wasiwasi wa jumla juu ya usalama wa wahudumia misaada ya kiutu waliopo Darfur, ambao wingi wao waliamrishwa kuhama eneo hilo, kufuatia tangazo la tarehe 04 Machi la Mahakama ya ICC la kutaka kumshika Raisi Omar AlBashir wa Sudan kwa madai ya kuwa anahusuika na makosa ya vita na jinai dhidi ya utu katika Darfur. Lakini juu ya mazingira yote hayo, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la UNAMID hali, kijumla, kwa sasa hivi katika Darfur ni ya utulivu na ni shwari.