Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malawi inasonga mbele kujitegemea chakula

Malawi inasonga mbele kujitegemea chakula

Taifa la Malawi limepania kujitegemea kwenye zile shughuli za kuzalisha chakula, kwa madhumuni ya kuepukana na ile hali ya kigeugeu inayozisumbua zaidi zile nchi masikini zenye kutegemea kufadhiliwa mchango wa chakula kutoka mataifa ya kigeni. Kuweza kulitekeleza lengo hilo Serikali ya Malawi iliamua kuchangisha mchango maalumu kutoka bajeti ka kitaifa, ikisaidiwa na UM, kuimarisha shughuli za kilimo nchini ambazo hudhibitiwa kwa taratibu zenye kuwasaidia zaidi wakulima wadogo wadogo.

Malawi imewekeza fungu kubwa la bajeti, kwenye huduma za kilimo, kwa makusudio ya kukuza uzalishaji chakula nchini na, hatimaye, kujivua milele na baa la njaa.

Kwa maelezo zaidi kuhusu ripoti juu ya juhudi za Malawi katika kudhibiti bora kilimo kwa natija za umma wote nchini, sikiliza idhaa ya mtandao.