Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Tume ya UM ya Kuratibu na Kukadiria Maafa katika Namibia (UNADC) imeeleza kwenye ripoti iliokabidhiwa Serikali na Timu ya Maofisa Wakazi wa Mashirika ya UM, kwamba katika ordha ya vitu vinavyohitajika kuchangishwa kidharura, kukidhi mahitaji ya umma ulioathirika mafuriko yaliotukia karibuni nchini, ni pamoja na chakula, huduma za afya, maji safi na salama pamoja na makazi na mazingira ya usafi.

 Kadhalika, mashirika ya UM yametoa ombi la kutaka yaongezewe wafanyakazi ziada wanaotakiwa kusaidia huduma za kihali kwa umma muhitaji katika Namibia. Takwimu za UM zinaonyesha idadi ya watu waliong'olewa makazi na mafuriko imeongezeka sasa hivi na imefikia 54,581. Kadhalika ripoti ilisema mafuriko yalisababisha uharibifu mkubwa kwenye madaraja na barabara, maafa ambayo huzorotisha huduma za kupeleka misaada ya kihali kwa waathirika 344,000 waliosambaa katika sehemu kadha za nchi.

Mazungumzo ya UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani yaliofanyika Bonn, Ujerumani yamekamilisha duru nyengine ya matayarisho ya mkutano mkuu utakaokusanyisha Mataifa Wanachama Copenhagen, Denmark miwsho wa mwaka. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM ya UM juu ya Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (UNFCCC), amesema kikao kilichomalizika kimewawezsha wajumbe wa kimataifa kupata ufahamivu mzuri na kushuhudia uwazi wa kuridhisha, hali ambayo itasaidia vikao vya duru ijayo ya mkutano wa matayarisho, utakaofanyika tena Bonn mwezi Juni. Miongoni mwa mada ziolizosailiwa ni pamoja na taratibu zinazotakikana kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwenye juhudi za kupunguza umwagaji wa hewa chafu na katika kurekibisha athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, kwa ujumla.