Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa KM ataka kuchukuliwe hatua kali kimataifa dhidi ya uharamia Usomali

Mjumbe wa KM ataka kuchukuliwe hatua kali kimataifa dhidi ya uharamia Usomali

Wapatanishi wa Kimarekani wameripotiwa kujihusisha kwenye mazungumzo na maharamia wa Kisomali, ili kumwachia kapteni wa meli ya Marekani aliyeshikwa sasa hivi kwenye mashua ya kuokolea iliopo katika Bahari ya Hindi.

Kapiteni huyo, anayeitwa Richard Phillips, alinyakuliwa kutoka meli ya shehena ya kampuni ya Maersk Alabama, ambayo ilitekwa, kwa muda mfupi na maharamia. Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah amelaani msururu wa vitendo vya uharamia vilivyopamba karibuni nje ya mwambao wa Usomali. Alisema uhalifu wa aina hii ni lazima ukomeshwe na usiruhusiwe kamwe, na jamii ya kimataifa kufanyika, bila ya kuadhibu wale wote wanaohusika na uharamia. Alipendekeza kuongezwa kwa idadi ya manowari za kimataifa zenye kufanya doria kwenye eneo husika ili kuimarisha hifadhi bora ya zile meli za shehena, za kimataifa, na alionya bila ya kufanya hivyo maharamia husika wataendelea kukashifu na kuharimisha kanuni za kimataifa bila kukhofu adhabu.