Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisa wa Haki za Binadamu wa UM aipongeza FNL Burundi kwa kuwaachia huru watoto wadogo

Ofisa wa Haki za Binadamu wa UM aipongeza FNL Burundi kwa kuwaachia huru watoto wadogo

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto kwenye Mazingira ya Mapigano ameripotiwa kuyakaribisha maamuzi ya wanamgambo wa FNL Burundi, ya kuwatenga watoto 112, ikijumlisha watoto wa kike wawili, kutoka kundi hilo na kuwavua na hatari ya kushirikishwa kwenye mapigano.

FNL imeripoti pia kuwa inajiandaa kuwaachia huru watoto 200 wengine ziada mnamo siku za karibuni.