Skip to main content

Sudan Kusini yaanzisha sheria ya kuhifadhi haki ya mtoto

Sudan Kusini yaanzisha sheria ya kuhifadhi haki ya mtoto

Raisi wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit alitazamiwa leo kuthibitisha rasmi, utekelezaji wa Sheria mpya ya Haki za Mtoto kwa Sudan Kusini.

Raisi wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit alitazamiwa leo kuthibitisha rasmi, utekelezaji wa Sheria mpya ya Haki za Mtoto kwa Sudan Kusini. Peter Crowley, Mkurugenzi wa Operesheni za Mradi wa Maendeleo ya Watoto Sudan Kusini, unaoendelezwa kieneo na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) amezipongeza juhudi hizi za serikali kujenga jamii ambayo itahakikisha watoto huwa na fursa ya kukua na kustawi kimaisha, kwa kutumia kila uwezo waliojaaliwa kimaumbile, na kuhakikisha pia watoto hawa wanatekelezewa haki ya kupata huduma za afya, ilimu na huduma nyengine za msingi. Kadhalika, sheria hiyo itahakikisha watoto wanakuwa na uhuru wa kusema, na watabarikiwa uwezo wa kupata habari na maarifa, na pia kuhakikisha wanatunzwa na kuhifadhiwa dhidi ya unyanyasaji na makandamizo. Sheria ya Haki ya Mtoto Sudan Kusini imetafsiri mtoto kuwa ni mtu ye yote chini ya umri wa miaka 18, na matabaka ya sekta zote za Serikali Sudan Kusini yamelazimika kisheria kutambua haki za mtoto, na kuwajibika kuzihishimu na kuhakikisha haki hizo zinatekelezwa kama ilivyoidhinishwa ndani ya Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki ya Mtoto.