Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama linazingatia hali Guinea-Bissau

Baraza la Usalama linazingatia hali Guinea-Bissau

Baraza la Usalama limekutana asubuhi kuzingatia ripoti ya KM kuhusu usalama na amani katika Guinea-Bissau, na pia kusailia shughuli za Ofisi ya UM inayohusika na Ujenzi wa Amani nchini humo.

Joseph Mutaboba, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Guinea-Bissau  aliwasilisha mbele ya kikao cha hadhara cha Baraza la Usalama, ripoti juu ya hali ya vurugu na fujo zilizopamba katika kipindi cha karibuni nchini. Alibainisha kuwepo maafikiano ya jumla miongoni mwa raia wa Guinea-Bissau yenye kupendekeza uchaguzi wa taifa ufanyike tarehe 28 Juni mwaka huu, kufuatia mauaji ya Raisi pamoja na Mkuu wa Maafisa Washauri wa Makamanda wa Jeshi yaliotukia tarehe mosi Machi 2009. Mutatoba alisisitiza duru za fujo na vurugu nchini zinaweza kukopmeshwa, pamoja na ile tabia ya kufanya makosa ya jinai bila kujali adhabu, pindi patabuniwa tume maalumu itakayohusika na uchunguzi wa matukio kama hayo. Alipendekeza kwa wajumbe wa Baraza la Usalama kupeleka ujumbe maalumu kwa Vikosi vya Usalama na Serikali ya Guinea Bissau wa kuwakumbusha unaooelezea dhamana walionayo kisheria ya kulinda umma na kuwatekelezea haki za kibinadamu kikamilifu.