Tume ya UM juu ya Askari wa Kukodi yakamilisha uchunguzi Afghanistan

Tume ya UM juu ya Askari wa Kukodi yakamilisha uchunguzi Afghanistan

Wajumbe wa UM wa Tume ya Kazi kuhusu matumizi ya Askari wa Kukodi, inayowakilishwa na Amada Benavides de Perez na Alexander Nikitin, imekamilisha ziara ya uchunguzi, ya siku tano katika Afghanistan baada ya kujadiliana na maofisa wa Serikali pamoja na wadau wengine husika kuhusu upeo na hali halisi ya shughuli za Majeshi ya Binafsi na Kampuni za Ulinzi na Usalama ziliopo Afghanistan sasa hivi na namna shughuli hizo zinavyoathiri utekelezaji wa haki za binadamu kitaifa.