Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkariri wa UM kuhusu mauaji nje ya mahakama ashtumu vyombo vya sheria Kenya

Mkariri wa UM kuhusu mauaji nje ya mahakama ashtumu vyombo vya sheria Kenya

Profesa Philip Alston, aliye Mkariri Maalumu wa UM dhidi ya Mauaji Nje ya Taratibu za Mahakama amewasilisha ripoti ilioshtumu vikali vyombo vya sheria Kenya, ambavyo alidai hushiriki kwenye vitisho vya mpangilio na mabavu dhidi ya watetezi wazalendo wa haki za binadamu, hasa wale watetezi waliotoa ushahidi kwa tume ya uchunguzi ya UM juu ya ukiukaji wa haki hizo.

 Kwa mujibu wa Profesa Alston "darzeni za watetezi mashuhuri wa haki za binadamu nchini, ambao wanahishimiwa kitaifa, walisumbuliwa na kampeni za vitisho zilizoendelezwa na polisi na wanajeshi dhidi yao, kwa lengo la kuwafunga midomo, wao pamoja na jumuiya za kiraia zenye kugombania haki za binadamu" wasitoe ushahidi kwa UM juu ya uharamishaji wa haki za binadamu kwenye taifa lao. Idadi kubwa ya watetezi hawa inaripotiwa sasa hivi wamelazimika kwenda mafichoni nchini Kenya, na baadhi yao wameamua kuhama nchi kutafuta usalama. Alisema vitendo vya vitisho vinavyoendelezwa na polisi na wanajeshi Kenya, dhidi ya wapigania haki za binadamu, kutoruhusu kutoa ushahidi kwa wajumbe wa tume za uchunguzi za UM juu ya matukio, ni vitimbi vinavyokiuka kanuni za haki za msingi.