Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Uamuzi wa Kamisheni ya Uchaguzi wa Taifa Sudan (NEC) wa kufanyisha uchaguzi mkuu wa nchi katika mwezi Februari 2010, ni tangazo liliopokelewa kwa ridhaa kuu na KM, na amekitafsiri kitendo hicho kuwa ni kigezo muhimu katike utekelezaji wa Maafikiano ya Jumla ya Amani nchini.

Ujumbe wa makadirio kuhusu mahitaji ya kihali kwenye zile sehemu zinazodaiwa kama Maeneo Matatu ya Mtafaruku Sudan, umeanza kusailia athari kwa umma baada ya uamuzi wa mwezi Machi wa Serikali ya Sudan, kubatilisha ruhusa ya kazi dhidi ya mashirika 13 ya kimataifa, yasio ya kiserikali, na pia kupiga marufuku mashirika matatu mengine ya kizalendo, yasio ya kiserikali. Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kwamba kazi za tume zilianzishwa Alkhamisi katika Jimbo la Blue Nile. Ujumbe wa tume hiyo unajumlisha wawakilishi wa Serikali ya Sudan ya Muungano wa Taifa, Kamati ya Maeneo Matatu pamoja na Umoja wa Mataifa.

Kadhalika, Tume ya Umoja wa Afrika (UA) juu ya Darfur, yenye kuwakilisha Watu Mashuhuri wa Ngazi za Juu, inayoongozwa na Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki imewasili Al fasher, Darfur Kaskazini Ijumaa. Wajumbe wa Tume walikutana, kwa mashauriano, na viongozi wa Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) pamoja na maofisa wa Serikali ya jimbo. Mbeki alisema ziara yao ilikusudiwa hasa kukutana na umma wa Sudan, kwa dhamira ya kutafuta njia za kuridhisha ili kuharakisha taratibu za kuleta upatanishi, haki na amani kwa wote, kote nchini.

Victoria Tauli-Corpuz, Mwenyekiti wa Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili, akijumuika na wakariri/watetezi wa UM kuhusu haki za wenyeji wamekaribisha, kidhati, zile taarifa zlizobainisha kwamba kuanzia leo Australia imejiunga na orodha ya Mataifa Wanachama yalioridhia Mwito wa UM kuhusu Haki za Wenyeji wa Asili Duniani. Mnamo Septemba 2007 Australia ilikuwa moja ya Mataifa manne yaliopinga Mwito baada ya kupitishwa na Baraza Kuu la UM. Wataalamu watatu wa Baraza Kuu, kwenye taarifa ya pamoja, wamesisitiza uidhinishaji wa Austarlia wa Mwito wa Haki za Wenyeji wa Asili ni kitendo kitakachoimarisha zaidi mwafaka wa jkimataifa kuhusu haki za wenyeji wa asili.