UM kuchangisha msaada wa kuihudumia Namibia kudhibiti athari za mafuriko

2 Aprili 2009

UM unajishughulisha hivi sasa kuchangisha dola milioni 2.7 zinazohitajika kuisaidia Jamhuri ya Namibia kudhibiti bora athari za mafuriko nchini, yaliosababishwa na mvua kali za karibuni ambazo zilin\'goa makazi watu 13,000 na pia kuharibu majumba na njia za kujipatia rizki kwa jumla ya watu 350,000.

Serikali imeshatayarisha kambi 21 katika majimbo sita nchini, kambi ambazo zitatumiwa kuwapatia makazi ya muda watu waliopoteza mastakimu kutokana na mafuriko. Idadi ya watu wanaohitajia uhamisho wa dharura wa makazi katika Namibia kwa sasa unaendelea kukithiri.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter