Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA imezikaribisha ahadi za Maraisi wa Urusi na Marekani kuzuia uenezaji wa silaha za kinyuklia duniani

IAEA imezikaribisha ahadi za Maraisi wa Urusi na Marekani kuzuia uenezaji wa silaha za kinyuklia duniani

Mohamed ElBaradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) ameingiwa matumaini makubwa na amezikaribisha ahadi za pamoja, zilizotolewa wiki hii na Raisi Dmitry Anatoleyevich Medvedev wa Shirikisho la Urusi pamoja na Raisi Barack Obama wa Marekani za kuchukua hatua hakika kutekeleza majukumu yao, chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Kinyuklia Duniani ili, hatimaye, kuuwezesha ulimwengu kuwa huru dhidi ya silaha za maangamizi ya halaiki za kinyuklia.

 ElBaradei alisema ahadi za maraisi hawa wawili za kufuatilia upunguzaji, wenye kuthibitika, wa akiba zao za silaha za kushambulia za kinyuklia, ni hatua itakayoharakisha utekelezaji ulizorota kwa muda mrefu wa mapendekeo ya ule Mkataba wa Jumla wa Kudumisha Upigaji Marufuku wa Majaribio Yote ya Silaha za Nyuklia ulimwenguni.