Skip to main content

Wahamiaji walionusurika mwambao wa Libya wameripoti ajali yao ilisababishwa na hewa mbaya na woga wa abiria

Wahamiaji walionusurika mwambao wa Libya wameripoti ajali yao ilisababishwa na hewa mbaya na woga wa abiria

Wale wahamiaji waliokolewa kutoka mashua ya wafanya magendo, iliopinduka mwanzo wa wiki nje ya mwambao wa Libya, wamewaambia wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ya kuwa boti yao ilizama kwa sababu ya matatizo ya hali ya hewa mbaya, ikichanganyika na woga pamoja na khofu kubwa iliowavaa abiria, walipogundua kuvuja kwa mashua yao.

 Watu walionusurka na ajali hiyo waliwaambia maofisa wa wa Shirika la IOM, pamoja na wale waliowakilisha Shirika la UM Linalohudumia Wahamiaji (UNHCR), kwamba mfanya magendo wa KiMisri aliyehusika na safari yao alifariki kwenye tukio hilo.