Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya majongoo ya pwani imepungua ulimwenguni, yahadharisha FAO

Idadi ya majongoo ya pwani imepungua ulimwenguni, yahadharisha FAO

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti ya kuwa akiba ya majongoo wa pwani, au madondo, inaelekea kupungua ulimwenguni kwa kima cha kushtusha, hasa katika maeneo ya Afrika na kwenye Bahari ya Hindi ambapo uvuvi wa majongoo hawa imekiuka ada.

Kadhalika katika sehemu za Pasifiki za bara la Asia, inasemekana majongoo hawa wameshamalizika au waliosalia ni kidogo sana. Majongoo wa pwani/madondo ni chakula cha jadi kwa wakazi wa bara la Asia, na hutumiwa kutengenezea supu, na kwenye vyakula vinavyokangwa na vinavyochemshwa. Mataifa ya Indonesia, Papua New Guinea na Philippines ndiyo yenye kusafirisha kwa wingi bidhaa ya madondo.