Skip to main content

UNDP inayahimiza mataifa ya kundi la G-20 kuzingatia mahitaji ya umma wa nchi masikini kwenye majadiliano yao

UNDP inayahimiza mataifa ya kundi la G-20 kuzingatia mahitaji ya umma wa nchi masikini kwenye majadiliano yao

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) wiki hii limetoa taarifa maalumu kwa viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la G-20, wanaokutana Alkhamisi mjini London, yenye kuwakumbusha ya kuwa mgogoro wa uchumi duniani huathiri zaidi maendeleo na maisha duni ya umma uliopo katika nchi masikini.

Taarifa ya UNDP ilisisitiza kwamba mzozo wa fedha na shughuli za mabenki katika nchi zenye maendeleo ya ufundi ndio zilizochochea mzozo huo na nchi tajiri zinawajibika kufanya kila ziwezalo kuhakikisha nchi masikini na zilizo dhaifu kiuchumi, ziliopo nje ya maeneo yao, huwa zinapatiwa usikivu unaofaa kwenye mijadala yao na kuzingatia uwezekano wa kuzifadhilia misaada ya kihali na mali ili kuziwezesha kuokoka na matatizo ya kiuchumi na jamii yanayotokana na mzoroto wa uchumi kwenye nchi tajiri.