Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

kwenye Mkutano Mkuu London na viongozi wa mataifa yenye uchumi mkuu, wanachama wa Kundi la G-20, uamuzi ambao waliahidi watachangisha furushi la dola trilioni 1.1, za kutumiwa kusuluhisha mzozo wa kiuchumi na fedha uliouvaa ulimwengu kwa hivi sasa. KM alitumai maafikiano ya G-20 yatayazipatia nchi masikini msaada maridhawa wa kufufua tena shughuli zao za maendeleo ya uchumi na jamii, kitaifa, kwenye maeneo yao.

 

 KM Ban Ki-moon amekaribisha uamuzi uliotolewa Alkhamisi Risala ya KM iliotolewa kufuatia majadiliano ya Kundi la G-20, ilibainisha kuwa mataifa wanachama "yalimthibitishia tena kwamba watatekeleza ahadi walizotoa siku za nyuma za kukuza mchango wa fedha zinazohitajika kuzisaidia nchi masikini kuyafikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia" kwa wakati katika 2015 ili, hatimaye, zipunguza ufukara na hali duni. KM alisema msaada huo utajumlisha dola bilioni 300 zitakazotumiwa mnamo miaka miwili ijayo katika nchi masikini.

Ripoti mpya ya KM kuhusu ulinzi amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) imerudia tena ule mwito wake kwa wajumbe wa Baraza la Usalama pamoja na zile nchi zilizochangisha wanajeshi wa kulinda amani kufadhilia vifaa, na pia zana zinazohitajika kukusanya taarifa za maadui pamoja na ndege na walimu wa mafunzo ya kijeshi, mahitaji ambayo yanatakiwa kuimarisha zaidi shughuli za vikosi vya amani vya UM katika JKK (MONUC), majeshi ambayo sasa hivi yameenezwa nchini mwisho wa kikomo cha uwezo.

Baraza la Usalama Alkhamisi limepitisha ajenda ya kazi chini ya uongozi wa Mexico, taifa liliodhaminiwa Uraisi wa Baraza kwa mwezi Aprili.