Skip to main content

KM-uchaguzi wenye kasoro hatari kwa Afganistan

KM-uchaguzi wenye kasoro hatari kwa Afganistan

KM Ban ki-moon ameonya kwamba uchaguzi utakaokua na kasoro huko Afghanistan utaweza kurudisha nyuma maendeleo yaliyopatikana, akitoa mwito kwa jumuia ya kimataifa kusaidia juhudi za kuimarisha uthabiti katika taifa hilo linalokumbwa na ghasia.

 Akizungumza kwenye kikao cha ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa juu ya Afghanistan huko The Hague Jumanne, alisema mara nyingi uchaguzi wenye kasoro hupelekea ukosefu wa utulivu zaidi na hili ni jambo lisiloweza kuruhusiwa kutokea huko Afghnaistan. Akiwa huko The Hague, Bw Ban alikutanana na Rais Hamid Karzai na kujadili juu ya uchaguzi wa rais ulopangwa kufanyika mwezi Augusti, pamoja na masuali ya demokrasia na jukumu la afisi ya UM huko Afghanistan UNAMA.