Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuungana na kamati kubuni mpya kazi za mazingira

UM kuungana na kamati kubuni mpya kazi za mazingira

Mpango huo unatokana na jibu kwa pendekezo la waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, wakati wa mkutano wa viongozi wa Jopo la Uchumi huko Davos, Uswisi mwezi Januari, wa kundwa kwa kamati maalum ya kupunguza kiwango kikubwa cha utowaji gesi za carbon.

 Kiasi ya makampuni 52 za biashara na watalamu 34 pamoja na mashirika mengine yamejiunga na kamati hiyo itakayofanya kazi na serekali na mashirika ya kimataifa kama lile la mazingira la UM, UNEP, kuchunguza namna ya kubuni mamilioni ya nafasi zinazohitajika kwa haraka za kazi za kijani na kuweza kuchochea ukuwaji wa uchumi utakaoelekea katika kupunguza kiwango cha kudumu cha kutoa carbon.