Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada kamili unahitaji kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria

Msaada kamili unahitaji kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria

Ni lazima kugharimia kikamilifu Fuko la Global Fund kuweza kupambana dhidi Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria ikiwa nchi zinabidi kufikia lengo la kumpatia kila mtu Duniani uwezo wa kujikinga kutokana na HIV, matibabu, msaada na kuhuduma alisisitiza mkuu wa Shirika la UM la kupambana na Ukimwi UNAIDS.

 Michel Sidibe mkurugenzi mkuu wa UNAIDS, aliwambia wafadhili na washirika wanaokutana huko Caceres Hispania, kwamba nchi nyingi zinategemea Fuko hilo kugharamia mipango yao ya Ukimwi, na kuongezea kusema nchi zinahitaji makadirio ya kuaminika ya fedha ilikuweza kuzingatia juhudi zao kufikia malengo ya kumptaia kila moja huduma. Taasisi hiyo inasema mchango wa wafadhili kwa kipindi cha 2008 hadi 2009 umefikia dola bilioni 9.5 ikiwa imepunguka kwa dola bilioni 4 kufikia maombi yaliyotarajiwa ya kiasi ya dola bilioni 13.5. Katika ujumbe wake Jumatatu, KM Ban Ki-moon aliwahimiza wafadhili kuwekeza katika kupambana na magonjwa hayo matatu hatari duniani.