Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuzorota ghasis huko Afrika ya kati kunasababisha maelfu kukimbia makazi yao

Kuzorota ghasis huko Afrika ya kati kunasababisha maelfu kukimbia makazi yao

Kuongezeka kwa mapigano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kumesababisha maelfu ya wakazi kukimbia kutoka makazi yao kufuatana na idara ya huduma za dharura ya UM.

 OCHA inaeleza kwamba ghasia hizo zinaweza kuhujumu maendeleo yaliyokwisha patikana kuelekea kugawanya madaraka kati ya serekali na makundi ya waasi. Mapigano mepya huko kaskazini magharibi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya majeshi ya serekali na kundi jipya la waasi la CPJP, yamesababisha kiasi ya watu 6 400 kukimbia ndani ya msitu na wengine elfu 9 kuvuka mpaka na kuingia Chad. Kaimu mratibu wa OCHA huko Chad, Mai Moussa Abari amesema wale walokimbia makazi yao na kupoteza kila kitu walokua nacho, wanahitaji hivi sasa hifadhi na msaada wa dharura. Ametoa mwito kwa serekali kuhakikisha kuna njia kwa wafanyakazi wa misaada kuweza kuwafikia wale wote walokimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo mpya.