Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeshtushwa na vifo vingi vya wahamiaji huko Mediterrenean

UNHCR imeshtushwa na vifo vingi vya wahamiaji huko Mediterrenean

Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR limeelza kushtushwa kutokana na ripoti za kufariki na kupotea mamia ya wahamiaji nje ya pwani ya Libya walipokua wanajaribu kutafuta maisha mepya Ulaya.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM linasema kufuatana na habari za mwisho kiasi ya boti tatu za biashara haramu zilikua zinawasafirisha mamia ya wahamiaji zilizama nje ya pwani ya Libya. Msemaji wa IOM Jean Philippe Chauzy alisema boti hizo dhaifu zilizama kutokana na kupakiza kupita kiasi, mvua kali na dharuba na upepo mkali.

"Kwa kawaida boti hizo huwa zinajaza sana hakuna vyombo vya usalama vya aina yeyote ndani yake, hata maboya, kwa sababu lengo lao ni kupakiza watu wengi iwezekanavyo, bila ya kujali usalama au hadi ya watu wanaosafiri kwenye maboti wanaotaka kuelekea Italy na kisiwa cha Lampedusa"

Maafisa wa usalama wa misri wanaripoti ajali ilitokea kiasi ya km 30 kutoka pwani ya Libya. Wanasema baadhi ya raia wa Misri waliokolewa na mili ya wa-Misri wengine 10 ili kua miongoni ya walofariki. Chauzy anasema wengi wa wahamiaji kwenye boti hizo wanaaminiwa walitokea katika nchi za Afrika kusini mwa Sahara na Afrika ya Kaskazini. Alisema, Libya ndiyo nchi amabyo wengi wa wahamaiji huelekea kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika. Anasema zaidi na zaidi sasa, wahamaiji kutoka Pembe ya Afrika wanawasili Libya na kufanya safari za kuhatarisha maisha yao kuelekea Ulaya.