Skip to main content

Hapa na pale

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amesema juhudi kubwa zaidi zinahitajika kote duniani kukomesha ghasia dhidi ya wanawake na wasichana, hasa kwa kuwahusisha zaidi wanaume na wavulana.

Mjumbe wa KM huko JKK Alan Doss amepongeza hatua ya kamati huru ya uchunguzi ya nchi hiyo kutangaza ratiba ya kutathamini utaratibu wa uchaguzi wa serekali za majimbo na mitaa. Kazi hizo zitaanza huko majimbo ya Kinshasa na Bas Kongo mwezi wa June na kuenea kote nchini humo hapo Augusti. Wakati huo huo Afisi ya UM huko DRC, MONUC imeripoti kwamba wapiganaji zaidi wa kundi la wanamgambo wa kihutu kutoka Rwanda FDLR, wanajiondowa kutoka kundi hilo.

Wanajeshi 100 kutoka Misiri waliwasili Darfur Jumatatu katika juhudi za kuimarisha kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na UM UNAMID huko Darfur. Wanajeshi wengine 100 walitarajiwa kuwasili siku ya Ijumanne wakati mkutano wa kamati ya pande tatu, serekali ya Sudan, AU na UM itakapokutana kwa mara ya kwanza huko Darfur.