Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kupambana na ukame pembe ya Afrika

FAO kupambana na ukame pembe ya Afrika

Kwa ushirikiano na Makundi yasiyo ya Kiserekali na Umoja wa Ulaya EU, Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, linafanya kazi kukabiliana na matatizo msingi yanyosababisha njaa huko Pembe ya Afrika.

Mchanganyiko wa mizozo iliyozuka mwaka huu kutokana hasa na ukame, kupanda bei za vyakula, migorogoro na ukuwaji wa wakazi ni miongoni mwa matatizo, lakini suluhisho la muda mrefu linahitajika imeeleza FAO. Katika ripoti yake ya mwisho ya mwezi uliyopita juu ya mzozo wa Pembe ya Afrika, UM umeonya kwamba kiasi ya watu milioni 19.8 watahitaji msaada wa dharura katika kanda hiyo licha ya kwamba kumekuwepo na mavuno mazuri kutokana na mvua zilizotokea huko sehemu za Somalia, Kenya na Ethopia. Mwakilishi wa Idara ya Huduma za Dharura za EU pembe ya Afrika Lammert Zwagstra anasema, ili kuweza kunusurika na kuishi kawaida kila mfukaji anahitaji kwa wastani mifugo minne, idadi ambayo anasema imepungua kutokana na kuongezeka idadi ya wakazi hasa wanaoshindania mifugo michache iliyopo na maji machache, mbali na hali mbaya ya ukame, mabadiliko ya hali ya hewa na ghasia. Kwa ushirikiano wa pamoja EU, FAO na Mashirika yasiyo ya Kiserekali wameanza juhudi za kuhakikisha maji yanapatikana katika maeneo kwa kawaida hayana maji, kuchimba visima, kusaidia ufugaji, kutoa huduma za afya na masomo juu ya afya ya mifugo, pamoja na kusaidia jamii katika njia za kuzuia migogoro.