Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Annan atoa mwito wa hatua za haraka za mageuzi Kenya

Annan atoa mwito wa hatua za haraka za mageuzi Kenya

Viongozi wa kisaisa kutoka Kenya na wa Mashirika yasiyo ya Kiserekali wanakutana mjini Geneva, kutokana na mwaliko wa KM wa zamani wa UM Kofi Annan kujadili juu ya matokeo ya utawala wa muungano nchini humo, baada ya ghasia zilizotokea kufuatia uchaguzi mkuu wa Disemba 2007.

Akiufungua mkutano huo wa siku mbili Bw Annan Mpatanishi Mkuu wa makubaliano ya kugawanya madaraka huko Kenya alisema, hatu za polepole za kufanya mageuzi ya mambo yaliyokubaliwa yamewavunja moyo wa-Kenya wa kawaida. Bw Annan amesema ingawa wa-Kenya mwanzoni waliunga mkono mpango wa mageuzi lakini wamekasirishwa na kukerwa na ugomvi katika Baraza la Mawaziri na kutoweza kuundwa Mahakama Maalumu kuwafikisha mahakamani walohusika na ghasia baada ya uchaguzi. Hata hivyo Bw Annan alisema kuna matumaini mambo kubadilika ikiwa hatua za haraka na thabiti zitachukuliwa kufanya mageuzi ya katiba, bunge, mahakama uchaguzi na mageuzi ya mashamba.